Cristiano Ronaldo ameendelea kufanya vyema katika soka baada ya kufunga jumla ya mabao 916 katika michezo 1200 aliyocheza mpaka sasa.Mshambuliaji huyo anayekipiga Al Nassr ya nchini Saudi Arabia amekuwa na mwendelezo mzuri kwa msimu huu akifunga mabao 16 katika michezo 19 aliyocheza mpaka sasa.
Ronaldo amekuwa na mwendelezo mzuri kwa mwaka 2024 akifunga jumla ya mabao 43 katika mechi 51 alizotumikia Klabu ya Al Nassr na timu yake ya taifa ya Ureno. Mpaka sasa Ronaldo anahitaji mabao 84 pekee ili aweze kufikisha mabao 1000 na kuweka historia ya kuwa mchezaji wa kwanza Duniani kufikia rekodi hiyo.
Mbio za Ubingwa wa EURO NATIONAL LEAGUE
Ureno wamefanikiwa kufika robo fainali ya ligi ya Ulaya na watavaana na Switzerland na kama watashinda mchezo huo watakutana na Ujerumani ama Ufaransa katika hatua ya nusu fainali. Katika michuano hiyo Ronaldo hajafanikiwa kufunga bao lolote.Ronaldo anategemea kuwa miongoni mwa wachezaji wa Ureno watakaocheza michuano ya kombe la Dunia mwaka 2026 nchini Marekani akiwa na umri wa miaka 41 na yatakuwa ni mashindano yake ya mwisho kushiriki.
Kuihama Al Nassr na kujiunga Al Hilal
Ronaldo anahusishwa kuhamia klabu ya Al Hilal kama mbadala wa Neymar Jr anayekumbwa na majeraha ya mara kwa mara. Ronaldo alisajiliwa na Al Nassr kwa mkataba wa Paundi milioni 175 na mkataba wake unamalizika june 2025. Taarifa zisizo rasmi zinasema Ronaldo anaweza kujiunga na Al Hilal ili aweze kucheza michuano ya kombe la dunia kwa vilabu inayohusisha timu 32 kutoka mabala yote.
Ni hatua ambayo inaweza kumfanya Lionel Messi wa Inter Miami akashiriki uwanja na Ronaldo kama walivyofanya kwa miaka mingi nchini Uhispania kwa Barcelona na Real Madrid.
Kama Ronaldo atajiunga na Al Hilal basi atakabiliana na timu yake ya zamani Real Madrid waliopangwa kundi H pamoja na Al Hilal,RS Salzburg na Pachuca.