Johansen Buberwa – Kagera.

Madereva wa magari yanayobeba Wanafunzi Nchini, wametakiwa kuwa makini wanapokuwa barabarani, ili kuepusha matukio ya ajali.

Wito huo, umetolewa na Kamanda wa Kikosi cha Uusalama Barabarani Nchini, Ramadhan Ng’anzi katika ziara yake ya siku mbili Mkoani kagera na akizungumza na madereva wanaoendesha magari ya shule.

Amesema, “Wazazi wanawaamini Madereva na kuwapata Watoto wao wawapeleke shuleni na baadae kuwarejesha nyumbani salama mnapaswa kutambua kuwa mnadhamana kubwa ingawa kuna baadhi yenu mmelalamikiwa kufanya vitendo vya udhalilishaji kwa watoto.”

Katika ziara hiyo, pia Ng’azi amefanya uzinduzi wa zoezi la ukaguzi wa magari hayo kwa msimu mpya wa mwaka 2025 na kusema kuwa wanafunzi wapo katika rika ambalo bado linahitaji uangalizi wa hali ya juu.

Msamaha wa Rais wawanufaisha Wafungwa 83 Kagera
Ghorofa laporomoka, kuna vifo na majeruhi