Johansen Buberwa – Kagera.
Wafungwa 83 kutoka Magereza mbalimbali Mkoani Kagera, wamenufaika na msamaha wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan alioutoa Desemba 9, 2024.
Taarifa hiyo, imetolewa na Kaimu Mkuu wa Magereza Mkoani Kagera, Hezron Norbeth wakati akizungumza na Waandishi wa Habari.
“Kati ya Wafungwa hao, watatu wamesamehewa na kuhachiwa huru na wafungwa 80 wamepunguziwa sehemu ya hadhabu ya vifungo vyao,” amesema ACP Norbeth.
Hata hivyo, Norbert amewataka Wafungwa waliochiwa huru kuhakikisha wanaishi vizuri na jamii na kuepukana na kufanya makosa ambayo yanaweza kuwapelekea kurudishwa Gerezani.