Takribani Watu wasiopungua 127, wengi wao wakiwa ni raia wameuawa nchini Sudan kufuatia mapigano kati ya jeshi na Wanamgambo wa RSF.
Taarifa za vyombo vya Habari zinasema wengi wao wameuawa katika mji wa Omdurman huku wengine zaidi ya 100 wakiuawa katika soko la Kaskazini mwa mji wa Kabkabiya huko Darfur.
Gavana wa Khartoum, Ahmed Othman Hamza amesema kombora lililorushwa na Wanamgambo hao wa RSF lilipiga basi la abiria na kuwaua watu wote 22 waliokuwamo.
Hata hivyo, pande mbili ambazo zimekuwa zikipambana tangu Aprili mwaka 2023 zimeshutumiwa kushambuliana vikali kwa makombora na kuyalenga maeneo ya raia, ambayo yanayokaliwa na watu wengi.