Wizara ya Afya ya Nchini Misri, imearifu vifo vya Watu wanane ambao wamepoteza maisha baada ya Ghorofa kuporomoka jijini Cairo.
Taarifa iliyotolewa na Wizara hiyo imeeleza kuwa kuporomoka kwa jengo hilo la la Ghorofa sita katika kitongoji cha Waili Magharibi mwa Cairo pia kumesababisha watu watatu kujeruhiwa.
Hata hivyo bado haijafahamika chanzo kilichosababisha jengo hilo lililojengwa miaka ya 1960 kuporomoka, ingawa Ofisi ya Gavana iliarifu kuanza kwa uchunguzi unaoratibiwa na waendesha mashtaka.
Kuporomoka kwa majengo ni jambo la kawaida nchini Misri, Inaarifiwa kuwa ujenzi duni na ukosefu wa matengenezo ya majengo nchini humo umekuwa ukisababisha majengo mengi kuporomoka na hali hii imezoeleka.

Madereva Mabasi ya Wanafunzi wapewa somo kuepuka ajali
Wizara ya Mambo ya Ndani wampokea Bashungwa