Kiongozi wa juu wa Iran, Ayatullah Ali Khamenei amesema kuanguka kwa Rais Bashar al-Assad wa Syria wiki iliyopita kuliwa ni mpango na mkakati wa Marekani na Israel.

Khamenei ambaye ni Kiongozi mwenye nguvu kubwa ya kisiasa nchini Iran, amesema nchi yake ina ushahidi unaothibitisha kwamba kupinduliwa kwa Rais Assad ulikuwa mpango wa Mataifa hayo mawili na jirani mmoja wa Syria, ambaye hakumuweka wazi.

Hata hivyo, Wachambuzi wanasema nchi hiyo huenda ikawa ni Uturuki, ambayo imekuwa ikipambana na wale inaowaita magaidi kwenye mpaka wake na Syria kwa miaka mingi.

Iran, ambayo ilikuwa mshirika mkubwa wa utawala wa Assad, inatajwa kuwa mmoja wapo wa waathirika wakubwa wa kuporomoshwa kwa utawala huo, kupitia Muungano wa Mapambano, ambao unaongozwa na taifa hilo kwa ushirikiano na Yemen, Syria, makundi ya Hizbullah nchini Lebanon na Hamas katika Ukanda wa Gaza.

Madereva mabasi yanayozidisha mwendo kukiona
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Desemba 12, 2024