Askari wa Usalama Barabarani wametakiwa kukamata mabasi yanayoendeshwa kwa mwendokasi mara tu wanapoona kosa hilo kupitia mfumo wa VTS na wasisubiri mpaka orodha ya mabasi yaliyovunja sheria kutoka Makao Makuu ya Polisi pekee.

Hayo yameelezwa Desemba na Mrakibu Msaidizi wa Polisi ( ASP) Mwashamba Onesmo kutoka KIkosi cha Usalama Barabarani Makao Makuu alipokuwa akitoa elimu kwa askari maeneo ya Stand Kuu ya Mabasi iliyopo Misuna, Kata ya Misuna, Wilaya na Mkoa wa Singida.

Naye, Koplo wa Jeshi la Polisi Chambo ambaye aliambatana na ASP Onesmo, alitoa elimu kwa askari juu ya jinsi ya kutambua madereva ambao wamechezea ving’amuzi vyao na kuwachukulia hatua.

Urusi yawashauri Raia wake kutoenda Marekani
Anguko la Al-Assad: Marekani, Israel zimehusika - Khamenei