Serikali ya Nchi ya Urusi imewataka raia wake kutosafiri kwenda Marekani, Canada au baadhi ya nchi za Umoja wa Ulaya, ikisema kuna hatari ya kuandamwa na mamlaka za Marekani, kutokana na uhusiano mbaya uliopo kati yao.

Taarifa ya Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi, Maria Zakharova imeeleza kuwa uhusiano wa Urusi na Marekani uko katika hali ya hatari ama kuvunjika kabisa.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi, Maria Zakharova.

Uhusiano huo uliingia dosari kufuatia uvamizi wa Urusi nchini Ukraine na ulifikia kiwango kibaya zaidi mwezi uliopita baada ya Ukraine kuanza kutumia makombora ya masafa marefu ya Marekani na Uingereza.

Vitendo vya udhalilishaji: Polisi waisaidie jamii - Pembe
Madereva mabasi yanayozidisha mwendo kukiona