Jeshi la Polisi Mkoa wa Kusini Pemba, limetakiwa kuendeleza mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili na udhalilishaji wa wanawake na watoto kwa kuwakamata na kuharakisha kukamilisha upelelezi wa kesi hizo na kuwafikisha wahalifu hao mahakamani ili wachukuliwe hatua stahiki zitakazokomesha vitendo hivyo.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa maendeleo ya jamii, jinsia,wazee na watoto, Riziki Pembe Juma alipokuwa akizungumza na Wananchi pamoja na wadau mbalimbali wanaojihusisha na mapambano dhidi ya vitendo hivyo katika Maadhimisho ya siku 16 ya kupinga vitendo vya ukatili na udhalilishaji wa wanawake na watoto.

Amewataka Wananchi na wadau hao kutoa ushirikiano wa dhati kwa Jeshi la Polisi pamoja na kuwa tayari kwenda kutoa ushahidi mahakamani pale itakapobidi kufanya hivyo.

Aidha ameitaka jamii kuondoa muhali na kakubali kufanya suluhu katika vitendo hivi vya ukatili na udhalilishaji kwani kufanya hivyo kunamkosesha muathirika haki yake na hupelekea kuongezeka kwa vitendo hivyo.

Maadhimisho hayo ya siku 16 za kupinga vitendo vya ukatili na udhalilishaji wa wanawake na watoto yamefanyka katika kiwanja cha kufurahishia watoto Tibirinzi Chake Chake Pemba.

Urusi yawashauri Raia wake kutoenda Marekani