Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo – CHADEMA, Tundu Lissu ametangaza rasmi nia ya kugombea nafasi ya Uenyekiti wa Chama hicho Taifa, nafasi ambayo kwa sasa inashikiliwa na Freeman Mbowe.

Tundu Lissu amesema tayari amewasilisha taarifa kwa Katibu wa Chama kuondoa kusudio la kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti na badala yake atagombea nafasi ya Mwenyekiti wa Chama.

Amesema, “ni kweli, nimekuwa Makamu Mwenyekiti [CHADEMA] kwa miaka mitano iliyopita, na nimekuwa kwenye Kamati Kuu kwa miaka 20.”

Lisu ameongeza kuwa, “hii miaka 20 imenipa fursa ya kutosha ya kufahamu wapi panavuja, wapi panahitaji marekebisho, wapi panahitaji maboresho.”

Mazingira: Wadau wa Maji, Sekta Mtambuka wakutana Moro
Vitendo vya udhalilishaji: Polisi waisaidie jamii - Pembe