Johansen Buberwa – Kagera.
Mkuu wa Wilaya Bukoba Erasto Sima ameagiza Kamati ya Ualama ya Wilaya hiyo kuanza ukaguzi wa haraka wa Makampuni yote yanayohusika kutoa ajira ya ulinzi, ili wapatikane wenye sifa na vigezo hasa waliopita jeshi la Akiba au Jeshi la Kujenga Taifa, JKT.
Sima ameyasema hayo wakati akihitimisha mafunzo ya ya Askari wa Akiba 68 katika kambi ya muda iliyokuwa katika shule ya Msingi Mbembe Wilaya Bukoba kata Kemondo Halmashari ya Bukoba na kusema kuna baadhi ya makampuni ya ulinzi yemeajiri watu amvao hawajapitia mafunzo kama hayo.
“Mwaka jana wakati manispaa ya Bukoba wakati tunahitimisha mafunzo ya Mgambo kabla ya miezi mitatu minne tulitoa furusa kwa makampuni hayo ili kuwapatia nafasi watu ambao hawajapitia mafunzo wawapeleke wakahitimu mafunzo ili waendelee kufanya kazi kwao na zipo baadhi ya kampuni zilipeleka watumishi wao kuanzia leo tuanze kufanya ukaguzi kwenye makampuni yanayofanya ulinzi kwenye wilaya yetu ya Bukoba,” amesema Sima.
Awali akisoma taarifa ya wahitimu hao, Donatus Cleophace Byabato amesema jeshi hilo linakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ajira, kukosa ushirikiano kati ya vyombo vya ulinzi na usalama, kudharauliwa na Raia na kuomba fursa zitakapopatikana wapewe kipaumbele.
Kwa upande wake Mshauri wa Jeshi la akiba wa Wilaya hiyo, Luteni Kanali Nimrod Ezekiel Kitinya amesema mafunzo hayo yatawasaidia Vijana kuwa wakakamavu na kuwaweka tayari kwa ulinzi wa Taifa pamoja na uzalendo
Amesema, mafunzo hayo yalianza Mei 27, 2024 na kuhitimishwa Desemba 11, 2024 yakiwa na na jumla ya wahitimu 68 wakiume 61 na saba wa kike na baadhi yao walikuwa na sifa za kwenda kulijenga Taifa.
“Wahitimu walifundishwa kwata, uraia, usalama wa Taifa, Usalama wa raia, umuhimu wa vyombo vya habari na madhara yake, ujasiliamali, rushwa, ugaidi pamoja na silaha.