Baada ya aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo – CHADEMA Taifa bara, Tundu Lissu kutangaza kuwania nafasi ya Uenyekiti Taifa wa chama hicho, makundi kadhaa yenye nguvu yameibuka kuitaka nafasi ya Umakamu Uenyekiti ambayo sasa ni rasmi iko wazi.

Vyanzo vya kuaminika ndani ya Chama hicho vinaeleza kuwa makundi hayo ni lile la aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Taifa (BAVICHA) John Heche Mwenyekiti wa kanda ya Mashariki anayemaliza muda wake na swahiba mkuu wa Mwenyekiti wa Taifa (Mbowe) Godbless Lema na Mwenyekiti wa Kanda ya Victoria Ezekiel Wenje.

Taarifa za ndani ya kambi hizo zinaeleza kuwa vita ni kubwa kutokana na kila mmoja kuonekana kuwa na uswahiba wa namna moja ama nyingine na Mwenyekiti wa sasa Freeman Mbowe, hali ambayo inakiweka chama hicho kwenye kupasuka vipande pale hatua ya mchujo itakapowadia, na hatimae Uchaguzi wenyewe wa kumpata Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa.

Wasifu wa Vijana wa makundi haya tukianza na John Heche yeye alianzia kwenye nafasi ya Uenyekiti wa Baraza la Vijana (BAVICHA) kisha kuwa Mbunge wa Tarime kwa miaka mitano (2015-2020) baadaye kuwa Mwenyekiti wa Kanda Serengeti.

Godbless Lema yeye alianza kuwa mwanachama wa kawaida kisha Ubunge jimbo la Arusha Mjini na hatimaye Mwenyekiti wa Kanda ya Mashariki.

Ezekiel Wenje, Ubunge Nyamagana kwa miaka mitano, kisha Uenyekiti wa kanda ya Victoria nafasi ambayo anaishikilia hadi sasa.

Timu ya majadiliano Mradi LNG yafanya ziara ya mafunzo Indonesia
Ajira: DC Sima ataka ukaguzi Makampuni ya Ulinzi