Viongozi wa kundi la G7, wamesema wapo tayari kusaidia mchakato wa kipindi cha mpito nchini Syria, utakaoongozwa kwa utawala wenye kuaminika.

G7 imeeleza kuwa, mabadiliko ya kisiasa baada ya kumalizika utawala wa kimabavu wa Bashar al-Assad, unapaswa kuheshimu utawala wa sheria, haki za binadamu kwa wote.

Aidha, Viongozi hao pia wamezitaka pande zote kulinda uadilifu wa eneo la Syria na umoja wa kitaifa na kuheshimu uhuru na mamlaka yake.

Hata hivyo, Serikali mpya ya Syria imesema katiba na Bunge la nchi hiyo vitasitishwa kwa muda wa miezi mitatu, katika kipindi hiki cha mpito.

Tanzania, Indonesia zajadili fursa za uwekezaji Nchini
Taarifa za uhalifu ni siri, msizitoe kwa wenza wenu - Katabazi