Klabu ya Chelsea imeendelea kufanya vyema katika mbio za kuwania Ubingwa wa EPL baada ya kuibuka na ushindi wa mabao2-1 dhidi ya Brentford. Katika mchezo huo Marc Cucurela alikuwa wa kwanza kufngua nyavu za Brentford akimalizia pasi kutoka kwa Madueke dakika ya 43 ya kipindi cha kwanza na mpira kwenda mapumziko wakiwa kifua mbele.

Dakika ya 80 Chelsea walirejea tena langoni mwa Brentford na kuandika bao la pililililowekwa kimiani na Nicolas Jackson akimalizia pasi kutoka kwa Enzo Fernandez.Matokeo hayo yanawafanya Chelsea kuwa na alama 34 katika michezo 16 waliyocheza mpaka sasa wakishika nafasi ya pili nyuma ya Liverpool wenye alama 36 katika michezo 15.

Enzo Maresca na mbio za  ubingwa kimya kimya 

Kocha wa Chelsea Enzo Maresca amekuwa ni mwindaji wa ubingwa asiye na kelele. Kocha huyo amekuwa mwiba mkali kwa wapinzani wa Chelsea kwa kuwafunga mara 10 sare 4 na kupoteza michezo miwili pekee.Kocha huyu raia wa Italy ameisuka upya chelsea tangu alipokabidhiwa majukumu hayo mwanzoni mwa msimu chini ya Mmiliki wake Todd Boehly.

Uwezo mkubwa wa kuwaongoza wachezaji vijana kama Enzo Fernandez,Nicolas Jackson ,Cole Palmer umeifanya Chelsea kufunga mabao 37 ya EPL na kuruhusu mabao 19 pekee katika michezo 16.Chelsea ndiyo kinara wa ufungaji kwa sasa wakifuatiwa na Tottenham wenye mabao 36.

Ni Chelsea pekee iliyoshinda mechi tano zilizopita wakifuatiwa na Liverpool na Arsenal walioshinda mechi 3 katika michezo mitano iliyopita.

Wiki chache zilizopita Liverpool alikuwa kileleni kwa tofauti ya alama 9 na Arsenal walioshika nafasi ya pili lakini kwa sasa wanatofautiana alama 2 pekee na Chelsea.

Simba njia nyeupe kufuzu robo fainali Shirikisho
Amad Dialo aijeruhi City dakika za jioniii