Klabu ya Simba imeendelea kuonyesha ubabe wake ndani ya Dimba la Benjamin Mkapa baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya CS Sfaxien ya Tunisia katika mchezo wa kundi B Kombe la Shirikisho Africa. Matokeo hayo yameifanya Simba kuwiana alama na fc Bravos na Constantine wote wakiwa na alama 6 timu zote zikicheza michezo 3.

Tathmini ya Mchezo 

Simba chini ya Fadlu ilanza na Camara,Fabrice Ngoma,Jean Ahoua,Ateba Lionel,Abdulazak Hamza ,Mohammed Hussein,Debora Fernandes,Che Malone Fondo ,Awesu Awesu na Kibu Denis.  Katika mchezo hupo mgumu na wenye ushindani mkali Hazem Hassen wa Cs Sfaxien alikuwa wa kwanza kuipa timu yake bao la uongozi dakika ya tatu ya mchezo lakini Kibu Denis aliisawazishia Simba bao hilo dakika ya 7 na kuzifanya timu hizo kwenda mapumziko zikiwa na sare ya 1-1

Kipindi cha pili dakika ya 90+7 Kibu Denis alirejea tena langoni na kuipa Simba bao la pili la ushindi na kuifanya timu hiyo kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Ubora wa Kibu Denis 

Kibu Denis aliibuka nyota wa mchezo kwa mabao hayo mawili maridadi .Mbali na mabao hayo nyota huyo alionekana kuwa makini nyakati zote za mchezo akisaidia eneo la kiungo na mabeki wake. Uwezo aliouonyesha ndani ya mchezo umemfanya aimbwe na kila shabiki wa Simba na wengi wamemtabiria makubwa ndani ya kikosi hicho.

Malengo ya Simba msimu huu

Klabu ya Simba ilijiwekea malengo yake kimataifa kwa msimu huu ni kufika nusu fainali au kuingia fainali ya michuano hiyo.Hilo linawezekana kwa sababu mpaka sasa timu inaalama za kutosha kuweza kufuzu hatua ya robo fainali.Simba itakuwa na michezo miwili ugenini dhidi ya Cs Sfaxien na Bravos. Kisha itamaliza mchezo wake wa makundi dhidi ya CS Costantine katika dimba la Benjamini mkapa.

Watumishi Madini tambueni dhamana mliyopewa - Dkt. Kiruswa 
Enzo Maresca anavyorudisha ubabe wa Chelsea kimya kimya