Manchester United imesema kwamba inamuuza mshambuliaji wa Uingereza Marcus Rashford, 27, na itaidhinisha uhamisho wa bei ya chini Januari. (Gurad, nje

Mshambulizi wa Liverpool na Misri Mohamed Salah, 32, anakaribia kusaini mkataba mpya na klabu hiyo. (Marca – Spanish)

Southampton wanafikiria kumnunua meneja wa Sheffield Wednesday, 35, Mjerumani Danny Rohl baada ya kumfukuza meneja Russell Martin. (Times – Subscription Required)

Uhamisho wa majira ya kiangazi kuelekea Bayern Munich, Real Madrid au Manchester City kwa sasa haupo mezani kwa Mjerumani mwenye umri wa miaka 21 na kiungo wa kati wa Bayer Leverkusen Florian Wirtz, ambaye anatazamiwa kuongeza mkataba wake hadi 2028. (Sky Germany),

Winga wa Uingereza Raheem Sterling, 30, hana mpango wa kukatiza uhamisho wake wa mkopo katika klabu ya Arsenal licha ya kuhangaika kwa dakika za kawaida. (Standard)

Beki wa Arsenal Jakub Kiwior, 24, ameamua kuondoka The Gunners mwezi Januari, huku Napoli ikimtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa Poland. (Il Mattino – In Itali)

Manchester United inamsaka mshambuliaji wa Olympiacos ya Ugiriki Charalampos Kostoulas, 17. (Sun}

Ofa ya Brighton ya pauni milioni 20.7 kwa ajili ya Mbrazil Vitor Reis, 18, imekataliwa, huku Palmeiras ikiwa tayari kujadili mustakabali wa beki huyo baada ya Kombe la Dunia la Vilabu. (ESPN Brazil – In Portuguese), nje

.

Chanzo cha picha,Getty Images

Maelezo ya picha,Jacob Kiwior

Arsenal inamfuatilia kwa karibu kiungo wa Sevilla na Ufaransa Lucien Agoume, 22, kama mbadala wa kiungo wa kati wa Ghana Thomas Partey, 31. (FootballTransfers)

Mshambulizi wa Al-Ittihad ya Ufaransa Karim Benzema, 36, anafikiria kustaafu mapema mwishoni mwa msimu wa 2024-25. (Relevo – In Spanish),

Kiungo wa kati wa zamani wa Uhispania Cesc Febregas, ambaye sasa ni meneja wa Como, amempa mchezaji huru Mwingereza Dele Alli, 28, fursa ya kufanya mazoezi na timu yake kuanzia Januari huku kiungo huyo akiomba kufufua soka lake. (ESPN), nje

Kipa wa Ujerumani Manuel Neuer, 38, anatazamiwa kuongeza kandarasi yake na Bayern Munich kwa mwaka mwingine. (Sky Germany)

Maisha: Kisa uonevu nasingiziwa kesi ya Ujambazi
Vita Urusi, Ukraine: Ni lazima tukomeshe umwagaji damu - Trump