Na Mwandishi Wetu – Dar es Salaam.
Kampuni ya michezo ya kubashiri ya LEONBET imewazadia washindi wa kampeni ya Shangwe la Sikukuu zawadi kibao kwa kushiriki kampeni hiyo.
Kampeni hiyo iliyoanza kwa kishindo, mpaka sasa imeshuhudia wateja wa LEONBET wakishindia zawadi za simu janja au Smartphone, Smart TV inchi 65, na Pikipiki mpya.
Mkazi wa Njombe, Freddy Mbilinyi na Juliuz Ohimo wa Kigamboni jijini Dar es Salaam kila mmoja ameshinda pikipiki mpya.
Mbali ya pikipiki, pia mkazi wa Chamazi, jijini Dar es Salaam, Ally Juma aliibuka mshindi wa Smart TV inchi 65 huku washindi wengine 15 wakishinda zawadi ya simu janja au Smartphone.
“Washindi hawa ni ushahidi kuwa Shangwe La Sikukuu siyo ndoto bali ni fursa halisi ya kushinda zawadi mbalimbali msimu huu wa sikukuu ,” alisema meneja chapa wa kampuni ya LEONBET, Lizy Ngowi.
Lizy alisema kuwa kampeni hii ni mwanzo tu wa msimu wa furaha kwani Shangwe La Sikukuu ndo kwanza linazidi kushika kasi, na zawadi bado ni nyingi.
Alisema kuwa LEONBET imedhamiria kuhakikisha msimu huu wa sikukuu wateja wao wanaburudika ipasavyo mbali ya kushinda zawadi mbalimbali.
“Nawaomba wateja au mashabiki wa soka kubashiri na LEONBET ili kushinda zawadi nono. Kushiriki ni rahisi sana, ni kujisajili na LEONBET kupitia tovuti yetu na kuanza kubashiri kwenye mechi yoyote ama kucheza mchezo wowote unaopenda na kujiweka katika nafasi ya kushinda zawadi zetu,” alisema Lizy.
Alifafanua kuwa kila beti inakupa nafasi ya kuingia kwenye droo ya ushindi papo hapo.
Kwa mujibu wa Lizy, zawadi bado zipo nyingi kwani Shangwe La Sikukuu bado linaendelea.
“Usikubali msimu huu wa sikukuu upite bila kujishindia zawadi nono. Jiunge na familia ya LEONBET leo na ufurahie msimu wa sikukuu kwa namna ya kipekee,” alisema.
Alisema kuwa wateja wanaweza kutembelea tovuti ya LEONBET kwa maelezo zaidi na kuanza safari ya ushindi.