Ajali ya Lori la mizigo kugongana na Basi dogo la Abiria aina ya Coaster, zimesababisha vifo vya watu 14 na wengine wanane kujeruhiwa,
Ajali hiyo imetokea eneo la Mikese lililopo Barabara kuu ya Morogoro – Dar es salaam usiku wa Desemba 18, 2024 ambapo Lori hilo lilikuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea Morogogoro na Coaster iliyokuwa inatokea Morogoro kwenda Dar es salaam.
Akithibitisha kupokea miili ya marehemu hao, Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa Mkoa Morogoro, Nkungu Daniel amesema waliofariki bado hawajatambulika na majeruhi wanaendelea na matibabu.
Amesema, kati ya watu hao waliofariki Wanaume ni wanane na Wanawake ni sita huku Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima, akiwataka Wananchi kufikia Hospitalini hapo, Ili kutambua wapendwa wao.