Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa STAMICO, Dkt. Venance Mwasse amefanya mazungumzo na Kamishina wa Magereza Zanziba Khamis Khamis ili kufanikiza azma ya kuachana na matumizi ya kuni na kutumia nishati safi ya kupikia.

Dkt. Mwasse amefanya mkutano huo ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Pia alifanya mkutano  na Katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Dkt. Islam Salum kujadili namna wanavyoweza kuisaidia jamii visiwani Zanzibar kufikiwa na nishati safi kupikia.

Kwa upande wake Kamishina huyo wa Magereza Khamis ameahidibushirikiano ili kufanikisha Magereza kuhamia katika matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia.

Maisha: Skudu sasa kapona, ni Mwanaume kamili
Wazazi jela maisha kwa kutesa, kuuwa mtoto