Michuano ya Dar24 Chandimu Cup imeendelea kwa raundi ya pili robo fainali katika dimba la Msufini Chamazi ukizikutanisha Videte Academy dhidi ya Mzinga FC mchezo uliomalizika kwa Videte Academy kushinda mabao 6-0 na kuingia hatua ya nusu fainali kwa kishindo.
Kikosi cha Videte Academy kilichoshinda mchezo
Tathmini ya Mchezo
Kijana Ismail Mlilo maarufu kama Tepsi kutoka VIDETE ACADEMY ndiye aliyekuwa nyota wa mchezo baada ya kufunga mabao matatu katika ushindi wa mabao 6-0. Mabao mengine ya Videte Academy yalifungwa na Yulius Mlope,Sabri Hemed na Said Said. Mchezo huo ulimalizika kwa Clean sheet ya kwanza katika michuano hiyo na Ismail Mlilo amekuwa mchezaji wa pili kufunga mabao matatu sawa na Mbumba wa 770 FC.
Kikosi cha mzinga kilichopoteza mchezo
Hatua zinazofuata baada ya mchezo
Videte Academy wamefanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali mchezo utakaowakutanisha na 770 FC siku ya alhamisi Disemba 19. Mshindi wa mchezo huo ataingia hatua ya fainali itakayopigwa dimba la Msufini siku ya Jumapili Disemba 22.
Wachezaji na Makocha watoa maoni kuhusu mchezo