Michuano ya Dar24 Chandimu Cup imeendelea kwa raundi ya Tatu ikiwakutanisha wenyeji wa mashindano Msufini FC dhidi ya Magole FC mchezo uliopigwa dimba la Msufini.Mchezpo huo mkali wenye ushindani mkali ulimalizika kwa Msufini kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 na kufuzu hatua ya nusu fainali.

Kikosi cha Magole FC kilichopoteza mchezo dhidi ya Msufini 

Tathmini ya Mchezo

Kikosi cha Msufini chini ya kocha Fela kiliundwa na Ally Makarani,Shukuru Msumi,Ben Nyamka,Husein Malolo Sele,Mick Kandambe,George,Hafidh Kwangaya ,Hassain Faizi na Adam Kizega. Kikosi hicho kiliisaidia Msufini kupata mabao mawili ya kipindi cha pili yaliyowekwa kimiani na Hafidhi Kwangaya . Mabao haya mawili yalipelekea kocha Fela kufanya mabadiliko kwa kuwapa nafasi nyota watano ambao ni Omary Omary,Chande ,Mbaraka,Mussa Mbegu na Kifaranga JR .

Kikosi cha Msufini kilichoshinda mchezo

Mabadiliko hayo yalipunguza kasi ya Msufini na Magole FC walirejea mchezoni kwa kasi na kujipatia bao la kufuta machozi kwa mkwaju wa penati.

Hatua zinazofuata baada ya Ushindi

Msufini FC inakuwa timu ya tatu kufikia hatua ya nusu fainali na itamsubiri mshindi kati ya Songas FC na Fede Boys kwenye mchezo wa raundi ya pili ya Nusu fainali itakayopigwa Ijumaa Disemba 20 Dimba la Msufini na mshindi wa mchezo huo ataingia hatua za fainali zitakazopigwa Disemba 22 huku aliyepoteza akicheza mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu Disemba 21.

 

Washindi shangwe la sikukuu la LEONBET wapatikana
Dkt. Biteko: Ichukieni rushwa, fanyeni kazi kwa bidii