Baadhi ya Wafugaji wa Kaunti ya Kajiado Nchini Kenya, wameapa kutoshiriki katika shughuli ijayo ya utoaji chanjo kwa mifugo huku viongozi wa kiislamu wakitaka serikali kufanya mazungumzo na raia kuhusu suala hilo.
Serikali ya Kitaifa kupitia Idara ya Ustawi wa Mifugo, imetangaza kuanzisha mpango wa utoaji chanjo kwa ng’ombe 22 milioni kuzuia ugonjwa wa miguu na midomo (FMD) na kondoo na mbuzi 50 milioni, dhidi ya ugonjwa wa Pes des Petits (PDP).
Rais William Ruto amekuwa akitetea mpango huo akisema chanjo hiyo ni salama na imetengenezwa Kenya, huku Viongozi wa upinzani akiwemo Kalonzo Musyoka wakipinga suala hilo kwa madai kuwa ina madhara.
Aidha, wamewaonya Wafugaji dhidi ya kuwasilisha mifugo wao kuchanjwa wakisema shughuli hiyo imedhaminiwa na Taasisi za kigeni za kufanya utafiti wa Dawa za Mifugo zenye chembechembe za kubadilisha maumbile ya mifugo.
Kwa upande wao Wafugaji walisema Serikali isiwalazimishe kuruhusu mifugo yao ipewe chanjo kwani huwa haifanyi lolote kuhusiana na changomoto zingine ambazo huwa zinawakabili.
credit@TaifaLeo