Kisukari ni miongoni mwa magonjwa yanayoongezeka kwa kasi ulimwenguni na ambayo tayari yameondosha uhai wa watu wengi.

Ugonjwa huu hutokana na kiwango cha sukari kwenye damu kuwa juu kutokana na matatizo ya uzalishaji au matumizi ya insulin, homoni inayodhibiti sukari mwilini.

Chanzo.

Zipo aina kuu mbili za kisukari:

1. Hutokea pale ambapo Kongosho hushindwa kuzalisha insulin na hali hii husababishwa na mfumo wa kinga kushambulia seli za kongosho ambapo huanza utotoni au ujanani.

2. Husababishwa na mwili kushindwa kutumia insulin vizuri hasa kutokana na lishe duni, uzito kupita kiasi na ukosefu wa mazoezi.

Hali hii hutokea zaidi kwa watu wazima, lakini kwasasa hata vijana wapo hatarini.

Chanzo kingine cha kisukari ni kisukari cha mimba (Gestational Diabetes), ambacho hutokea kwa baadhi ya Wajawazito.

Dalili.

Zinaweza kuwa zinazoonekana au zisizoonekana haraka, hivyo uonapo usipuuze bali wapi ukapate vipimo.

Lakini kwa dalili zinazoonekana haraka ni pamoja na-:

i. Kukojoa mara kwa mara.
ii.  Kiu isiyoisha hata baada ya kunywa maji.
iii. Njaa kupita kiasi.
iv. Uchovu wa mara kwa mara.
v. Kupungua uzito bila sababu.
vi. Vidonda kutopona haraka.
vii. Uoni hafifu au kutoona vizuri.
viii. Miwasho kwenye ngozi.

Kinga.

Hata hivyo zipo mbinu za kuzuia Kisukari maana Waswahili walinena Kinga ni bora kuliko tiba.

1. Lishe bora.

Kula vyakula vya nyuzi nyuzi kama mboga za majani, matunda, na nafaka zisizokobolewa na pia epuka vyakula vyenye sukari nyingi na mafuta.

2. Mazoezi.

Yao ya aina nyingi, lakiji waweza kutembea, kukimbia au kufanya mazoezi mepesi angalau dakika 30 kwa kila siku.

3. Kupunguza uzito.

Mara nyingi uzito kupita kiasi huongeza hatari ya kisukari, hivyo jitahidi kufanya jitihada za kupunguza uzito wa mwili wako kama umekuzidia.

4. Msongo wa mawazo.

Hili nalo ni la kuepuka, kwani msongo wa mawazo huathiri homoni mwilini na kuwa kisabahishi cha kungeza hatari ya kisukari.

5. Upimaji wa afya.

Hili linatakiwa kufanywa mara kwa mara ili kuweza kujua uhalisia wa afya ya mwili wako na kuchukua hatua stahiki, wengi wamekuwa wakichelewa tiba kwa kutopenda kupima afya mara kwa mara.

Madhara.

Kiuhalisia Ugonjwa huu wa Kisukari usipodhibitiwa unaweza kusababisha mambo yafuatayo-:

i. Mishipa ya damu na moyo.

Shinikizo la damu, kiharusi, na ugonjwa wa moyo na mzunguko hafifu wa damu unaosababisha vidonda visivyopona.

ii. Figo.

Figo kushindwa kufanya kazi (hitaji la dialysis au upandikizaji).

iii. Macho.

Kuoata upofu, glaucoma, na cataract.

iv. Mishipa ya fahamu.

Maumivu, ganzi, au kupoteza hisia (hasa miguuni).

v. Ngozi.

Maambukizi na vidonda visivyopona (hatari ya kukatwa viungo).

vi. Kingamwili.

Maambukizi ya mara kwa mara.

vii. Afya ya akili.

Msongo wa mawazo.

viii. Uzazi.

Kukosa nguvu za kiume kwa Wanaume na matatizo ya uzazi kwa Wanawake.

Tiba.

Kiukweli, kisukari hakina tiba ya moja kwa moja, lakini kinadhibitiwa kwa mfumo ufuatao-:

Aina ya kwanza ya Kisikari inahitaji
Matumizi ya sindano za insulin kila siku.

Na aina ya pili ya Kisukari kwa kubadili mtindo wa maisha.

Unashauriea pia kupata lishe bora na pia kuepuka matumizi ya vyakula vya sukari na mafuta mengi kama ilivyobaijishwa hapo awali

Mazoezi ya mara kwa mara (dakika 30 kila siku), na matumizi ya dawa za kisukari kulingana na ushauri wa daktari.

Londo: Halmashauri zichechemue fursa za Biashara mipakani