Watu 17 raia wa China (wote Wakiume) wamekamatwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo – DRC kwa tuhuma za kuendesha shughuli za uchimbaji madini katika mgodi haramu wa dhahabu.

Tukio hilo, limetokea katika mji wa Bukavu, wakati serikali ikiendelea kukabiliana na vitendo vya uchimbaji wa madini bila vibali na kwasas wanashikiliwa katika mji huo wa Jimbo la Kivu Kusini.

Waziri wa fedha wa Jimbo hilo na Kaimu Waziri wa Madini, Bernard Muhindo amesema watu hao walikamatwa baada ya ujumbe wa serikali kufanya ukaguzi wa kushtukiza walipotembelea eneo la mgodi katika kijiji cha Karhembo Desemba 19, 2024.

Amesema takriban raia 60 wa China na wengine kadhaa wa Kongo na Burundi walikuwa mgodini hapo, lakini maafisa waliamua kuwaweka kizuizini Wachina hao walioonekana kuwa ni wasimamizi.

Chanzo ajali ya Basi kuuwa 11 Kagera chatajwa
Tunahitaji Mtu wa kuwapambania Wananchi sio ahadi - Gavu