Takribani Watu 11 wamefariki dunia na wengine 16 kujeruhiwa baada ya Basi walilokuwa wakisafiria kufeli breki na kupata ajali katika Kijiji cha Kabukome kilichopo Kata ya Nyarubungo Wilaya ya Biharamulo Mkoani Kagera, hapo jana Desemba 21, 2024.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera Blasius Chatanda amelitaja Basi hilobni lile lenye za usajili T 857 DHW linalofanya safari zake kati ya Kigoma na Bukobavna kudai kuwa lilipinduka baada ya kuacha njia.

Amesema, waliofariki katika ajali hiyo ni Wanaume wanne Wanawake watano, Mtoto wa kiume mmoja na Mtoto wa kike mmoja na miili yote imehifadhiwa katika Hospitali teule ya Wilaya ya Biharamulo.

Kamanda Chatanda amesema, “Gari hili lilipotoka Biharamulo kwenda Bukoba lilipitiliza kituo cha kushuka Mtoto mmoja sasa Ndugu zake wakapiga simu kuwa wamempitisha, Dereva akakutana na Coaster kwenye mlima ule kwa sababu ya haraka akasimamisha gari mlimani konda akashuka na mtoto ili amuwaishe kwenye gari ambalo linawahi Biharamulo.”

“Kwa bahati mbaya mfumo wa gari ukagoma, mfumo wa breki mfumo wa gia vyote vikagoma gari likaanza kuserereka na likawa limemshinda Dereva likatoka nje ya barabara na kubinuka na Watu wengi wamepoteza maisha kwasababu walilaliwa na gari,” alibainisha Kamanda Chatanda.

Ajali iliyouwa 11: Bashungwa awajulia hali majeruhi 
Wachina 17 wadakwa kwa uchimbaji haramu wa Dhahabu