Tume ya Rais ya Kutathmini kuhusu Mgogoro wa Ardhi katika Hifadhi ya Ngorongoro imeundwa ambapo Jaji wa Mahakama ya Rufani, Dkt. Gerald Ndika ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wake ili kufanya tathmini kuhusu masuala ya ardhi yanayolalamikiwa na wakazi wa Hifadhi ya Ngorongoro.
Taarifa iliyotolewa kwa Vyombo vya Habari na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi, Dkt. Moses Kusiluka imeeleza kuwa, uteuzi huo unakuja baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kukutana na Viongozi wa kimila wa jamii ya kimasai wanaoishi eneo la Hifadhi la Ngorongoro Desemba Mosi, 2024 na kusema ataunda Tume mbili.
Ya Kwanza itafanya tathmini kuhusu masuala ya ardhi yanayolalamikiwa na wakazi wa eneo la Hifadhi ya Ngorongoro ambapo ile ya pili itaangalia utekelezaji wa zoezi la uhamaji wa hiari kutoka eneo la Hifadhi hiyo.
Majina ya walioteuliwa ni kama inavyoonekana hapa katika viambata.