Takriban Watu 11 wamefariki dunia na wengine 13 kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha Basi dogo la Abiria aina ya Coaster lenye namba za usajili T. 497 DZW na gari ya mizigo aina ya Fuso lenye namba za usajili T 707 EBZ iliyotokea Wilayani Handeni Mkoani Tanga.

Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Wakili Albert Msando kupitia taarifa yake ameeleza kuwa,  “Tarehe 25/12/2024 mida ya saa tatu usiku imetokea ajali eneo la Kwenkwale, Kata ya Kitumbi, Wilaya ya Handeni.”

Taarifa hiyo imezidi kufafanua kuwa, “ajali hiyo imehusisha magari ya Fuso T. 707 EBZ iliyokuwa inatoka Lushoto kuelekea Dar es Salaam na Coaster ya abiria T. 497 DZW iliyokuwa inatoka Mkata kwenda Tanga mjini.”

Waliofariki ni pamoja na madereva wa magari yote mawili na Majeruhi 13 wa ajali hiyo wanapatiwa matibabu Hospitali ya Wilaya ya Handeni.

Kuhusu hali ya majeruhi imedaiwa kuwa tisa kato yao bado sio nzuri na Miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Handeni.

Machafuko: Zaidi ya Wafungwa 1,500 watoroka Gerezani
Malimwengu: Bonde lililosheheni Sayari Libya