Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, George Katabazi amethibitisha taarifa za Mtoto Grayson Kanyenye (6), anayedaiwa kuuawa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani.
Kamanda Katabazi amesema, tukio hilo limetokea majira ya saa moja asubuhi katika mtaa wa Bwawani, Ilanzo Extension jijini Dodoma Desemba 25, 2024, nyumbani kwa Ofisa Uvuvi wa Mtera, Hamis Mohamed ambaye anatajwa kuwa mpenzi wa mama wa mtoto Zaituni Shaban ambaye ni maarufu kwa jina la Jojo.
Amesema, Hamis na Mama wa mtoto huyo walitoka kwenda matembezini na kumuacha chini ya uangalizi wa Dereva bodaboda, Kelvin Gilbert ambaye walimfahamu kupitia huduma ya usafiri anayoitoa kwa familia hiyo.
“Kelvin Gilbert aliachiwa mtoto huyo amwangalie, wakati Hamis na mama yake walipoondoka kwenda matembezini, lakini waliporudi saa moja kamili asubuhi walikuta mtoto Graison Kanyenye Mabuya amepigwa kichwani na kitu kizito kwenye paji la uso, huku akiwa na majeraha shingoni.”