Johansen Buberwa – Kagera.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Hajat Fatma Mwassa amesherekea sikuu ya krisimas na watoto wanaoishi katika mazingira magumu na wenye uhitaji maalumu Bukoba Mkoani Kagera akiambatana na Waandishi wa Habari na Timu kutoka Ustawi wa Jamii

Hajat Mwassa aliwaalika watoto hao zaidi ya 200 kutoka katika vituo vinne vya kulelea watoto yatima na wale wenye uhitaji vilivyoko katika Manispaa hiyo Desemba 25, 2024.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) jimbo la Bukoba mjini, Joas Muganyizi Zachwa amempongeza Hajat Mwassa kwa kuandaa hafla hiyo kwani ameonesha upendo na hekima.

Amesema, “umeamua kula na hawa wahitaji huu ni kuonyesha upendo wako ulivyo mkubwa kwa wanakagera na wananchi wa Wilaya ya Bukoba na mkoa mzima wana amani na kazi unazofanya za kuleta maendeleo.”

Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera – UVCCM, Faris Buruhani amesema Mwassa amefanya tendo la huruma na lenye baraka ambalo limewagusa watoto na jamii.

Nao baadhi ya watoto, akiwemo Rewina Paulo kutoka Nusuru Manispaa wameshukuru kwa upendo wa dhati aliouonesha Hajat Mwassa kwao na kumuomba aendelee kuwakumbuka.

Mchungaji afariki akijaribu kumtoa muumini mapepo
Glory Temple Tanga watoa tabasamu kwa makundi maalum