Takriban Watu tisa wamefariki dunia na wengine ambao idadi yao bado haijajulikana kujeruhiwa kufuatia ajali iliyohusisha basi la Ngasere na Noah Wilayani Rombo Mkoani Kilimanjaro kugongana uso kwa uso.
Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Raymond Mwangwala amethibiyisha kutokea kwa ajali hiyo ya hii leo Desemba 26, 2024.
Amesema idadi kubwa ya watu walifariki papo hapo na wengine wakati wakipatiwa matibabu na majeruhi bado wanaendelea kupatiwa matibabu.