Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameongeza hamasa kwa mabondia Watanzania baada ya kueleza kufuatilia moja kwa moja mapambano ya #KnockoutYaMama na kuwataka walipiganie Taifa lao.
Pambano hilo linaendelea jijini Dar es Salaam, ambapo bondia wa Tanzania atakayeshinda Mkanda wa Ubingwa kwa matokeo ya Knockout ataondoka na bonasi ya Sh 10milioni, huku atakayeshinda kwa pointi akiondoka na kitita cha Sh 5milioni na mabondia watakaoshinda kwenye mapambano yasiyokuwa ya ubingwa wakiondoka na zawadi ya Boxing Day Sh 1milioni kila mmoja.
Katika kukoleza ushindi kwa Watanzania, Rais Samia anayefuatilia pambano hilo laivu kwenye luninga, amepiga simu ukumbini na kutoa hamasa kwa mabondia Watanzania wanaozichapa usiku huu.
Kupitia simu ya Waziri Mkuu ambaye ni mgeni rasmi kwenye pambano hilo, Rais Samia alizungumza na mamia ya mashabiki na mabondia na kuwasisiziza kulipigania taifa leo.
“Nimesikia kuna mabondia kutoka nje ya nchi, mabondia wetu Watanzania mpewe bendera ya taifa na mpiganie taifa lenu,” amesisitiza Rais Samia.