Taifa la Tanzania bado lipo kwenye mikono salama baada ya Bondia Mtanzania, Mchanja Yohana kutembeza kichapo usiku huu kwa kumchapa makonde ya kutosha Bondia kutoka Philipino, Miel Fajardo.

Yohana ameshinda kwa pointi 116 kwa 111 za majaji wote watatu katika pambano la Raundi 12 la #KnockOutYaMama ndani ya ukumbi wa Super Dome Masaki usiku huu na kufanikiwa kushinda mkanda wa World Boxing Organization Global flyweight championship (WBO Global).

Kwa ushindi huo wa pointi, Mchanja anaondoka na kitita cha #KnockoutYaMama cha Shilingi Milioni tano (5 Milioni).

#KnockoutYaMama

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Desemba 27, 2024
Rais Samia: Mabondia wetu nawaangalia laivu, piganieni Taifa