Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kasimu Majaliwa, amepokea tuzo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyokabidhiwa na wadau wa ngumi nchini kwa kuthamini na kuendeleza sekta ya michezo nchini.
Waziri Mkuu pia amekabidhi tuzo kwa wadau wa Michezo kwa kuipigania sekta hiyo kwa jasho na damu akiwemo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paramagamba Kabudi na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Gerson Msigwa.
Majaliwa ametoa na kupokea zawadi hizo usiku huu wakati wa mapambano ya #KnockoutYaMama yakiendelea ndani ya ukumbi wa Super Dome hapa Masaki Jijini Dar Es Salaam.
#KnockoutYaMama