Watu wengi hulitumia Papai kwa sababu ya utamu wake lakini sina hakika endapo wote wanajua faida lukuki za tunda hili kwa afya ya mwanadamu.

Tunda la papai lina vitamini A,B,C,D, na E jambo linalofanya tunda hili kuwa katika kundi la matunda na vyakula vyenye utajiri mkubwa wa vitamini.

Inaaarufiwa kuwa kutokana na uzuri wa tunda hili, mvumbuzi maarufu, Christopher Columbus alilitaja tunda la Papai kama “Tunda la Malaika.”

Asili ya Papai ni Amerika ya Kati na kuanzia kwa matunda, majani na utomvu wa mmea huu, kiukweli hutumiwa kutengenezea dawa katika maeneo mbalimbali Ulimwenguni.

Vilevile, Tunda la Papai na utomvu wake hutumika kutengeneza pombe na mvinyo katika baadhi ya nchi, huku wengine wakitumia mpapai kutengenezea dawa kwa ajili ya mifugo na binadamu.

Hapa tutaangalia faida za Tunda la Papai na namna linavyotajwa katika kuimarisha afya ya Mwili wa Binadamu kiafya.

1. Papai lina vitamin C na vitamini A kwa wingi pia lina potassium na folate, ambapo tafiti zinaonesha kuwa antioxidant aina ya lycopene iliyomo kwenye Papai husaidia kuzuia saratani.

2. Tunda hili pia lina vitamin B, vitamin E na vitamin K. Pia lina madini ya calsium (kashiam) potassium, mgnessium na copper na pia punje zake ni dawa kwa baadhi ya matatizo ya ini na figo.

Papai pia lina protelytic enzymes ambayo husaidia kuuwa bakteria, minyoo na wadudu wengine hatari ndani ya tumbo katika mfumo wa umeng’enyaji wa Chakula.

3. Papai linatambulika kwa uwezo wake wa kuulinda mwili na maradhi ya uzee kama macho, misuli na kuzeheka kwa haraka.

Ndani yake kuna Zeaxanthin ambayo ni anti oxidant yenye kazi ya kuchuja miale hatari ya jua, ikiaminika kuwa antioxidant hizi husaidia katika afya ya macho na husaidia katika kudhibiti kudhoofu kwa misuli.

4. Aidha, Papai husaidia kupunguza hatari ya kuwa na ugonjwa wa pumu kwani ndani ya papai kuna virutubisho vingi, lakini uwepo wa beta-carotene ndani yake huwasaidia wagonjwa wenye pumu.

5. Antioxidanti zilizopo kwenye Papai husaidia l kupunguza athari za kupata maradhi ya saratani kwa Vijana na husaidia kudhibiti kupata saratani ya kwenye via vya uzazi hasa saratani ya korodani.

6. Ni kati ya matunda yaliyobeba vitamini K ambavyo ni muhimu katika afya ya mifupa, kwahiyo ulaji wa tunda hili husaidia kuimarisha afya ya mifupa.

Vitamin K pia husaidia ufyonzwaji wa madini ya calcium na huzuia upotevu wa madini haya kupitia mkojo.

7. Kwa mujibu wa Tafiti za kisayansi zinaonesha kuwa Papai ni Tunda linalofaa kwa wenye maradhi ya  kisukari, likiwa ni kati ya Matunda yaliyo kwenye kundi la Vyakula vyenye maji kwa wingi.

Hata hivyo, tafiti zinaonesha kuwa watu wenye kisukari hatua ya 1 wameweza kupunguza kiwango cha sukari mwilini na wenye kisukari hatua ya 2 wanaweza kuimarisha kiwango cha sukari mwilini pamoja na kiwango cha homoni.

8. Paipai pia lina enzyme zinazoitwa papain ambazo husaidia kumeng’enya chakula na kambakamba zake husaidia katika upatikanaji wa choo.

9. Madini ya potassium (aina ya chumvi) na vitamini vilivyomo kwenye Papai husaidia kulinda afya ya moyo na hatari inayoshambulia mfumo wa usukumaji wa damu mwilini.

Ulaji wa madini haya huku ukipunguza ulaji wa madini ya sodium (chumvi) husaidia kuulinda moyo dhidi ya maradhi hatari kama shambulio la moyo, presha na kiharusi.

10. Papai lina chembechembe ya Choline inayosaidia mwili hasa wakati wa kulala, kujongea kwa misuli (kukunja na kukunjuka, kutanuka na kusinjaa).

Pia husaidia kulinda mpangilio wa utando wa seli, husaidia katika kutunza kumbukumbu pamoja na wakati wa kusoma na pia husaidia katika ufyonzwaji wa mafuta mwilini.

Kiujumla Tunda la Papai lina faida nyingi na hata ukuaji wa nywele na kuzifanya zing’ae, hutokana na matumizi ya Papai kupona kwa vidonda, ukuaji wa tishu na ukuaji wa mwili kwa ujumla pia ni Papai, kutokana na kuwa Papai lina vitamin C na vitamin A.

Maisha: Nimekoma, sitawasogelea tena Changudoa - Dula
Polisi wakanusha kuwateka wakosoaji wa Serikali