Manchester United wameweka bei ya takriban £50m kumuuza mshambuliaji wa England Marcus Rashford, 27. (Caughtoffside), njeLiverpool wana uhakika mlinzi wa Uholanzi Virgil van Dijk, 33, ambaye mkataba wake unamalizika majira ya joto, atasaini mkataba mpya wa miaka miwili na klabu hiyo. (Team Talks)

Real Madrid hawana nia ya kumsajili Van Dijk msimu huu wa joto, licha ya ripoti kuwahusisha na Mholanzi huyo. (Marca – In Spanish)

Beki wa kushoto wa Bayern Munich Alphonso Davies, 24, yuko tayari kuhama Ligi ya Premia msimu huu, huku Manchester United na Liverpool zikiwa miongoni mwa vilabu vinavyomhitaji Mkanada huyo. (TBR Football)

Arsenal inamfuatilia mshambuliaji wa Wolves Mbrazil Matheus Cunha, 25, ambaye anaweza kupatikana ikiwa klabu hiyo ya Midlands itashushwa daraja kwenye Ubingwa. (Athletic – Subscription Required)

Winga wa Brazil Antony amekuwa na ofa za kuondoka Manchester United mwezi Januari lakini klabu hiyo haitaki mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 aondoke, kulingana na wakala wake. (Give Me Sport)

Wakala wa Dani Olmo amewasili Manchester huku klabu za Ligi ya Premia, zikiwemo Manchester United na Manchester City, zikitaka kuchukua fursa ya matatizo ya Barcelona kumsajili kiungo huyo wa kati wa Uhispania, 26, kabla ya tarehe ya mwisho ya Januari 1. (Mail)

.

Chanzo cha picha,Getty Images

Maelezo ya picha,Randal Kolo Mwani

Kuna “nafasi kubwa” ya mshambuliaji wa Paris St-Germain na Ufaransa Randal Kolo Muani, 26, ambaye amevutia Manchester United na Liverpool, kuhamia Ligi ya Premia Januari. (Football Transfers),

Fiorentina wanavutiwa na beki wa pembeni wa Parma mwenye umri wa miaka 25 Woyo Coulibaly. (Matteo Moretto – In Italy)

Kocha wa kikosi cha kwanza cha Liverpool John Heitinga anaongoza orodha ya watu wanaowania kuchukua nafasi ya Carlos Corberan kama kocha wa West Brom. (Football Insider)

Sporting Lisbon wanatazamiwa kujaza nafasi ya Joao Pereira, ambaye alitimuliwa siku ya Krismasi, na kocha wa Vitoria Guimaraes, Rui Borges. (Sky Sports) I

Mohammed Salah aweka rekodi mpya Liverpool ikijenga kiota kileleni
Watoto wa Mama Samia waiheshimisha Tanzania Kimataifa