Liverpool wameendelea kusalia kileleni mwa Ligi ya Premia kwa tofauti ya pointi saba baada ya kuifunga Leicester City 3-1 katika mchezo uliopigwa dimba la Anfield.

Jordan Ayew alifunga bao la kuongoza baada ya dakika sita pekee kwa upande wa Leicester, ambao baada ya kipigo hicho waliporomoka mpaka kwenye eneo la kushuka daraja.Dakika ya 45 Liverpool walisawazisha bao hilo kupitia kwa Cody Gakpo na timu hizo kwenda mapumziko kwa sare ya 1-1.

Dakika ya 49 Curtis Jones aliwainua mashabiki wa Liverpool baada ya kupachika bao la pili na Mohammed Salah aliikamilishia Liverpool ushindi kwa bao lake la tatu dakika ya 85. Matokeo hayo yameifanya Liverpool kufikisha alama 42 katika michezo 17 waliyocheza mpaka sasa.

Mohammed Salah anazaliwa upya 

Mohammed Salah amefanya mambo mawili makubwa katika mchezo dhidi ya Leicester City,Kwanza alifanikiwa kuongeza idadi ya bao katika kinyang’anyilo cha mfungaji bora akifikisha mabao 16 akiwa namba moja katika orodha ya wafungaji bora na pili ametimiza mabao 250 tangu alipoanza kucheza Ligi kuu ya Uingereza.

Ni mchezaji wa nne  kufikia mafanikio hayo kwa klabu moja, baada ya Wayne Rooney kwa Manchester United (276), Ryan Giggs kwa upande mmoja (271) na Harry Kane kwa Tottenham (259).

Salah pia ana mabao 100 ya Premier League ya nyumbani, huku 98 kati ya yale akifunga Liverpool na mawili Chelsea.

Yeye ni mchezaji wa nane tu kufikia hatua hiyo muhimu na amefanya hivyo katika michezo ya minne michache, baada ya Alan Shearer (mechi 91), Thierry Henry (113) na Sergio Aguero (125).

Nottingham Forest yatikisa,Manchester hapakaliki ,Chelsea yaharibu
Tetesi za Usajili Duniani Disemba 27