Wananchi wa kijiji cha Ipwaga wanaojishughulisha na shughuli za kilimo na ufugaji katika kata ya Mishamo, Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi, wametakiwa kuepukana na migogoro isiyo na tija na kuepuka kujichukulia sheria mkononi.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Tanganyika (OCD) Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Paul Mashimbi wakati akizungumza na Wananchi kwenye mkutano wa hadhara.

SSP Mashimbi aliwataka wananchi hao kupiga vita matukio yote ya ukatili wa kijinsia na kuyatolea taarifa Polisi ili hatua stahiki zichukuliwe kwa mujibu wa sheria.

Afya Tip: Zifahamu dalili za Kiharusi, Matibabu
Vyombo vya usalama vyakiri kuuwa Watu 10 kimakosa