Takriban Watu 10 wameuawa kimakosa wakati ndege ya jeshi la Nigeria iliyokuwa ikiwafuatilia majambazi katika vijiji viwili, ilipowashambulia katika jimbo la kaskazini magharibi la Sokoto.
Taarifa ya Gavana wa jimbo hilo, Ahmed Aliyu imeeleza kuwa raia wengine kadhaa walijeruhiwa kwenye mkasa huo na wengi wao wanatibiwa katika Hospitali huku kukiwa na taharuki.
Jeshi hilo, lilikuwa na dhamira ya kupambana na makundi ya wahalifu wenye silaha lakini waliwapiga mabomu kimakosa watu wasio na hatia.
Tayari Serikali imesema itachunguza operesheni hiyo ya kijeshi iliyosababisha vifo vya watu kwenye vijiji viwili vya Gidan Sama na Rintuwa kwenye jmbo hilo la Sokoto la magharibi mwa Nigeria.