Kiharusi.

Ni tatizo la ghafla la ubongo ambalo hutokea wakati mshipa wa damu kwenye ubongo wa binadamu inapoziba au kupasuka na kuvuja damu.

Sehemu hiyo ya ubongo huacha kupata damu na Tishu za ubongo ambazo hazipati damu huacha kufanya kazi na kufa, ambapo ikiwa tishu nyingi za ubongo zimeathiriwa, dalili zake huwa mbaya zaidi.

Aidha, endapo mshipa wa damu ulioziba utajifungua haraka, dalili zake zinaweza kutoweka kabisa na hii huitwa kiharusi cha muda mfupi (TIA), ambayo ni ishara ya tahadhari kuwa hivi karibuni unaweza kupata kiharusi.

Dalili.

i. Dalili za kiharusi huja ghafla, ambapo mtu hunapata dalili tofauti kulingana na sehemu ipi na kiasi gani cha ubongo wako kiliathiriwa

ii. Unaweza kuwa na ganzi ya uso au kulegea, mkono au mguu kuwa dhaifu, kutatizika kuona, matatizo ya kuongea au maumivu makali ya kichwa.

iii. Mara nyingi dalili za maradhi haya hujitokeza upande mmoja pekee wa mwili.

iv. Ingawa tishu za ubongo zinazokufa haziwezi kuwa hai tena, wakati mwingine sehemu zingine za ubongo wako huchukua kazi ya sehemu iliyoharibiwa.

iv. Ikiwa una dalili yoyote inayokufanya ufikiri kuwa una kiharusi, unapaswa kwenda Hospitali kupata huduma za dharura.

v. Matibabu na dawa yanaweza kusaidia kupunguza uharibifu wa ubongo na kuzuia kiharusi cha siku zijazo.

Sababu.

Kiharusi husababishwa na ukosefu wa mtiririko wa damu kwenye sehemu ya ubongo wako kutokana na:

i. Mshipa wa damu ulioziba kwenye ubongo

ii. Mshipa wa damu unaovuja damu kwenye ubongo wako

ii. Mshipa wa damu ulioziba unaweza kusababishwa na donge la damu ambalo hutokea kwenye mshipa wa damu kwenye ubongo.

iii. Damu kuganda kwenye moyo au mshipa wa damu karibu na moyo na kisha kuingia kwenye mtiririko wako wa damu na kukwama kwenye mshipa wa damu kwenye ubongo wako.

iv. Mrundiko wa mafuta (utando) ambao huvunja utando wa mshipa wa damu, husafiri hadi kwenye ubongo wako, na kukwama kwenye mshipa wa damu.

Tiba.

Madaktari hawawezi kurekebisha tishu za ubongo zilizoharibiwa na kiharusi lakini wanaweza kukupa matibabu ya:

– Dawa za kuvunja damu iliyoganda

– Kuondoa damu iliyoganda au kuziba mshipa unaovuja cha damu

– Kuzuia uharibifu wa ubongo usifikie kiwango kibaya zaidi kwa kurejesha mapigo ya moyo, shinikizo la damu na joto la mwili kuwa la kawaida.

-Ikiwa ulikuwa na damu iliyoganda, kuzuia kuganda kwa damu nyingine kwa kukupa dawa za kuyeyusha damu

– Kukusaidia kufanya kazi vizuri uwezavyo (kutumia tiba ya urekebishaji).

Hitimisho.

Nchini Marekani, takriban watu 795,000 wana kiharusi na takriban 130,000 hufa kutokana na kiharusi kila mwaka.

Kadiri kiharusi kinavyotibiwa haraka, ndivyo uharibifu wa ubongo unavyopungua na ndivyo uwezekano wa kupona unavyoongezeka.

Kwa kawaida, kadri unavyozidi kuimarika katika siku chache za kwanza, ndivyo utakavyoendelea kuzidi kuimarika.

Hivyo, kwa ujumla unaweza kutarajia kuendelea kuimarika kwa muda wa miezi 6 baada ya kuwa na kiharusi.

Aliyeuwa 27 aachiliwa huru, Raia wasema wanajua la kufanya
Wananchi epukeni migogoro isiyo na tija - SSP Mashimbi