Beki wa kulia wa Liverpool Trent Alexander-Arnold, 26, yuko mbioni kusaini mkataba na Real Madrid , huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza akiendelea kupuuza ofa mpya za kuongeza mkataba wake wa sasa unaomalizika msimu huu wa joto. (AS – in Spanish)

Liverpool itawanunua beki wa Bayer Leverkusen Mholanzi Jeremie Frimpong na beki wa Bayern Munich Alphonso Davies, wote 24, ikiwa Alexander-Arnold atajiunga na kikosi hicho cha Madrid. (Team talk)

h

Chanzo cha picha,Getty Images

Maelezo ya picha,Nigeria Ola Aina

Manchester City wanammfuatilia beki wa kulia wa kimataifa wa Nottingham Forest wa Nigeria Ola Aina, 28, kama kiungo mbadala wa Muingereza Kyle Walker, 34. (Sun)

Mshambuliaji wa Ureno na Al-Nassr Cristiano Ronaldo, 39, amekataa kukataa kuhamia Manchester City , licha ya kuwa amewachezea wapinzani wake Manchester United kwa misimu miwili. (Talksport)

Newcastle United wanavutiwa na beki wa kati wa Lens Abdukodir Khusanov kwa pauni milioni 25, lakini wanakabiliwa na ushindani wa kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Uzbekistan, 20, kutoka kwa wapinzani wa Primia Ligi Manchester City , Tottenham Hotspur , Leicester City na Wolves . (Cronicle)

Arsenal wanavutiwa na mlinda mlango wa Espanyol Joan Garcia, 23, lakini klabu hiyo ya La Liga inasalia kusisitiza kuwa kipengele cha kutolewa kwa Mhispania huyo cha pauni milioni 25 kilipwe. (Mirror)

Beki wa kushoto wa Crystal Palace Tyrick Mitchell, 25, hataki kuweka mustakabali wake wa muda mrefu katika klabu hiyo ya London, huku klabu ya La Liga Atletico Madrid ikimtaka Mwingereza huyo. (Caught Offside)

h

Chanzo cha picha,Getty Images

Maelezo ya picha,Martin Zubimendi

Manchester City hawana uwezekano wa kumfuatilia kiungo wa kati wa Uhispania Martin Zubimendi, 25, ambaye bado hataki kuhamia Uingereza kutoka Real Sociedad . (TBR Football)

Brighton wanapanga kumrejesha tena katika kikosi chao mlinda mlango Carl Rushworth mwenye umri wa miaka 23 kutoka kwa muda wake wa mkopo katika klabu ya Hull City huku kukiwa na nia ya kutaka kumnunua Muingereza huyo katika Ligi ya Premia. (Football Insider)

g

Chanzo cha picha,Getty Images

Maelezo ya picha,Glen Kamara

Southampton na Ipswich zote zina nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Rennes na Finland Glen Kamara, 29, mwezi Januari. (TBR Football)

Real Betis wako kwenye mazungumzo na wawakilishi wa kiungo wa kati wa Brazil Arthur, 28, kuhusu uhamisho wa mkopo kutoka Juventus . (Sport – in Spanish)

Liverpool yamaliza mwaka 2024 kwa kishindo
Ajali nyingine Nyasa: Sita wafariki wakiwemo Walimu wanne