Liverpool imeuaga mwaka 2024 kwa kishindo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Westham United. Liverpool chini ya kocha Arne Slot walianza na mfumo wa 4-2-3-1 ulioundwa na Allison Backer golini ,walinzi wakiwa ni Anold Trent ,Joe Gomes,Van Dijk na Robertson. Eneo la kiungo cha chini liliundwa na Mac Alister na Gravenberch. Eneo la kiungo cha juu liliundwa na Mohammed Salah,Jones na Gakpo wakati Luis Diaz alisimama kama mshambuliaji kiongozi.
Luis Diaz alikuwa wa kwanza kupachika nyavu za westham dakika ya 30 na bao la pili liliwekwa kimiani na Cody Gakpo dakika ya 40 na Mohammed Salah aliweka la tatu dakika ya 44. Mabao haya yaliwafanya Liverpool kwenda mapumziko wakiwa kifua mbele kwa mabao 3-0.Trent Alexander Anold alipachika bao la nne dakika ya 54 na bao la kufunga mwaka 2024 kwa Liverpool liliwekwa kimiani na Diogo Jota dakika ya 84.
Matokeo hayo yanawafanya Liverpool kusalia kileleni mwa ligi wakiwa na alama 45 katika mechi 18 walizocheza. Liverpool imepoteza mchezo mmoja pekee na sare 3.Huu ni mwanzo mzuri kwa kocha Arne Slot tangu alipowasili Anfield mwezi Julai na swali linabaki je ataweza kurudia hichi alichokifanya mwaka 2025?