Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama barabarani Mkoa wa Arusha, wanaendelea na ukaguzi wa magari ya Shule kwa lengo la kubaini changamoto na ubovu wa magari hayo, huku likibainisha kuwa litawachululia hatua za kisheria wamiliki na madereva wa ambao watakaidi zoezi hilo.

Akiongea wakati wa ukaguzi wa magari hayo Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, Zauda Mohamed amebainisha kuwa ukaguzi huo ulianza disemba mwaka jana mara baada ya wanafunguzi kufunga shule ili kuondoa usumbufu wanafunzi kipindi cha masomo.

Amesema, ukaguzi huo unafanyika kwa mujibu wa sheria ya usalama barabarani kifungu cha 39 sura 168 kama ilivyofanyiwa mapitio 2002 ambapo amewataka wamili na madereva kujitokeza katika zoezi hilo la ukaguzi wa vyombo vya moto kutokana na muda mchache uliobaki.

Aidha, amesisitiza kuwa atawachukulia hatua za kisheria wamiliki na madereva wote watakao kaidi kufanya ukaguzi wa magari ya shule kwa muda uliobaki sambamba na wale waliobainika vyombo vyao kuwa na changamoto wametakiwa kufanya marekebisho.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Desemba 3, 2024