Liverpool wako tayari kupokea ofa ya pauni milioni 50-60 kumuuza mshambuliaji wao wa miaka 25 wa Uruguay Darwin Nunez. (Football Insider)

AC Milan yaibuka kuwa klabu ya hivi punde kufikiria kumnunua mshambuliaji wa Manchester United Muingereza Marcus Rashford, 27. (Mail)

West Ham wanaandaa orodha ya washambuliaji wanaopania kuwasajili Januari hii ikiwajumuisha mshambuliaji wa Brighton wa Jamhuri ya Ireland Evan Ferguson, 20, mshambuliaji wa Wolves wa Korea Kusini Hwang Hee-chan, 28, na mshambuliaji wa Middlesbrough wa Ivory Coast Emmanuel Latte Lath, 26. (Telegraph – usajili unahitajika)

Maisha: Aonana na baba yake baada ya miaka 29
Afya Tip: Ufahamu Ugonjwa wa Usonji - dalili, tiba