Ac Milan imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Super cup ya Serie A baada ya kuwafunga mahasimu wao Inter Milan kwa mabao 3-2. Katika mchezo huo uliopigwa dimba la King Saudi University Stadium nchini Suadi Arabia uliishuhudia Inter Milan ikicheza kwa ufasaha na kujipatia mabao ya uongozi  dakika ya 45 kupitia kwa Laurato Morata na bao la pili dakika ya 47 kupitia kwa Mehdi Taremi.

Dakika ya 52 ya mchezo Ac Milan walirudi mchezoni kwa bao la Theo Hernandez, dakika ya 80 Christian Pulisic aliandika bao la pili na Tammy Abraham alipachika bao la ushindi dakika ya 90+3 na kuipa Ac Milan ubingwa wa Super Coppa.

Historia fupi ya Super Coppa

Michuano ya Super Coppa Italy ilianzishwa mwaka 1988 na awali ilihusisha timu mbili mpaka mwaka 2022 na kuanzia msimu wa 2023 timu ziliongezwa na kuwa timu 4. Klabu ya Juventus inaongoza kwa kutwaa ubingwa wa kombe hili ikitwaa mara 9 ikifuatiwa na AC Milan pamoja na Inter Milan zote zikitwaa mara 8. Lazio imetwaa ubingwa huo mara 5.

 

 

Guler awa gumzo Real Madrid ikiisambaratisha Deportiva Minera
Kagera: MSD yapewa tano uimarishaji wa ugavi bidhaa za afya