Matumizi ya takwimu sahihi yametajwa kuwa ni nyenzo muhimu katika kufanikisha kazi na majukumu ya kila siku ya Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii.

Hayo yamebainishwa Mkoani Morogoro na Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Lishe  kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI,  Luitfrid Nnally wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo ya kuwajengea uwezo  Wakufunzi kutoka vyuo vya Afya (HTis), vinavyotoa  Mafunzo ya Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii  pamoja na Waratibu wa Mikoa 12 na Halmashauri 25  kuhusu kitabu cha Mtua Namba 3.

Amesema, “watoa Huduma wa Afya Ngazi ya Jamii ili waweze kutumia vizuri nyenzo  na kuweza kuchukua taarifa kwa ajili ya kusaidia mambo mbalimbali  zitakazosaidia kuwaratibu vizuri na hizi taarifa zikiwa safi sana zitatuwezesha kutoa maamuzi  ambayo yanazingatia takwimu, maana yake mkiwafundisha vizuri watazingatia taratibu zote za kufanya kazi na kurahisisha ufuatiliaji hata kujua magonjwa yapo wapi, msimu gani , maeneo gani na hiyo inasaidia sana  kupeleka rasilimali mahali sahihi panapohusika.“

Aidha, ametumia fursa hiyo kuishukuru Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha kufanikisha Mpango Jumuishi wa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii uliozinduliwa tarehe 31, Januari, 2024 na Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango  ambapo sasa Wahdumu wa Afya Ngazi ya Jamii wanapata mafunzo katika vyuo mbalimbali vya afya  katika mikoa 11 na halmashauri 23 za mwanzo  katika kuhakikisha Watanzania wanakuwa na afya bora.

Kwa upande wake Mkurugenzi  wa  Ufuatiliaji na Tathmini  kutoka Wizara ya Afya  Cloud Kumalija amesema takwimu ni kiunganishi muhimu sana katika sekta ya afya.

“Takwimu ndio zinazotuunganisha sisi na dunia, Tanzania na WHO, na takwimu hutumika kutengeneza sera za Wizara na nini ni mstari wa mbele kutengeneza takwimu na asitumie muda mwingi kurekodi  atoe huduma lakini ahakikishe kinachorekodiwa ni sahihi na  matumaini yetu kuwa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii watasaidia sana kwenye eneo la Kinga,” aliongeza.

Kwa upande wake Mkufunzi wa Kitaifa wa Mafunzo ya Mtua Namba 3, Denis Kashaija amesema Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii ni watu muhimu hivyo kupitia mafunzo hayo yatarahisisha upatikanaji wa takwimu sahihi huku Mwalimu Mkufunzi wa Mafunzo  Sister Rucy Ifunyakufuatia takwimu kurahisisha kufanikisha mipango sahihi.

Marekani: Baridi yauwa watano, safari za anga zasitishwa
Guler awa gumzo Real Madrid ikiisambaratisha Deportiva Minera