Borussia Dortmund na Juventus wamejiunga na AC Milan katika mbio za kumnunua mshambuliaji wa Manchester United Muingereza Marcus Rashford, 27. (Sky Sports), kutoka nje.

Manchester City wanavutiwa na dili la kumsajili mshambuliaji wa Misri Omar Marmoush, 25, ambaye thamani yake inakadiriwa kuwa euro milioni 50 na ​​Eintracht Frankfurt. (Espn)

Lakini Eintracht bado hawajapokea ofa kutoka City kwa ajili ya Marmoush. (Sky Germany)

Omar Marmoush

Chelsea wanaongoza katika kinyang’anyiro cha kumsajili kiungo wa kati wa Uingereza Kobbie Mainoo, 19, ambaye mazungumzo yake ya kandarasi na Manchester United yamefikia tamati. (Mail)

Mainoo, ambaye mkataba wake unaendelea hadi 2027, hajaridhishwa na ofa ya awali ya Manchester United. (Manchester Evening News).

United wako tayari kumuuza mchezaji wao yeyote, akiwemo Mainoo, winga wa Argentina mwenye umri wa miaka 20 Alejandro Garnacho na mshambuliaji wa Denmark Rasmus Hojlund, 21. (Guardian)

Nottingham Forest wanajadili mpango wa kuongeza mkataba wa beki wa Brazil Murillo, 22, ambao kwa sasa unamalizika 2028. (Athletic – usajili unahitajika)

Palmeiras wana nia ya kumsajili kiungo mshambuliaji wa Brazil Andreas Pereira, 29, lakini bado hawajakubaliana na Fulham. (Fabrizio Romano)

Manchester United wanataka kumsajili beki wa Hungary Milos Kerkez lakini bei ya pauni milioni 40 ya Bournemouth kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 inaweza kuwa kikwazo. (Team Talk)

Borussia Dortmund inamfuatilia kiungo mshambuliaji wa Chelsea mwenye umri wa miaka 21 Carney Chukwuemeka. (Sky Germany)

Chukuemeka

Arsenal wanavutiwa na winga wa Athletic Bilbao Nico Williams, 22, lakini hawataweza kumnunua Mhispania huyo mwezi huu kwa sababu ya matatizo ya kifedha. (Talksport)

Southampton wanatarajia kumuuza beki wa Uingereza Kyle Walker-Peters, 27, ambaye mkataba wake unaisha msimu huu wa joto. (Football Insider)

Wamiliki wa Liverpool, Fenway Sports Group, hawajapokea ombi kutoka kwa mnunuzi yeyote wa klabu hiyo baada ya babake Elon Musk, Errol kusema kuwa mwanawe ana nia ya kuinunua Reds. (Sky Sports)

Maisha: Njia ya kuwashinda maadui katika ajira yako
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Januari 8, 2024