Kwa mujibu wa ripiti iliyotolewa Juni 10, 2019 na JAMA International Medicine, kwa mara ya kwanza kabisa kuwahi kutolewa duniani ilieleza uhusiano kati ya kuongezeka kwa uzito wa Wanawake na kulala kwenye vyumba vyenye mwanga mbadala (usio wa jua).

Ripoti hiyo, iliwatahadharisha Wanawake kuhusu kulala kwenye vyumba vyenye mwanga wa taa au mwanga wowote ule wa Luninga nyakati za usiku, ambao unaelezewa kuwa huongeza nafasi ya kupata vitambi na hivyo kujikuta wakijiuliza maswali ya kutosha yasiyo na majibu.

Aidha, ripoti hiyo pia ilitoa ushauri kwa Wanawake kwamba wanatakiwa kulala kwenye vyumba vilivyozimwa taa, yaani kulala gizani ili kuepukana na tatizo hilo linalowaletea kero kwa namna moja ama nyingine kwenye maisha yao ya kila siku.

Sehemu ya ripoti pia inaeleza kwamba,” Binadamu ameumbwa akizungukwa na mifumo ya mwanga wa jua nyakati za mchana na giza wakati wa usiku, hivyo mwili kupata mwanga usiku kunaweza kubadili mfumo wa utendaji kazi wa homoni pamoja na mifumo mingine iliyo shirikishi.”

Hata hivyo, ripoti hiyo haijaeleza kwanini athari hii inawapata wanawake pekee, sababu halisi ya kutokea kwa vitambi hivyo pamoja na utaratibu mzima wa namna ambavyo jambo hilo linafanyika na kwa hapa kwetu Tanzania Agosti 2019, Mkoa wa Kilimanjaro ulitajwa kuongoza kwa kuwa na Wanawake wenye vitambi, huku Dar es Salaam ikishika nafasi ya pili.

Usililojua: Binadamu huzaliwa na mkia
Mavazi ya Wakili yazua taharuki, kesi yaahirishwa