Manchester United wamefikia mkataba mpya na Amad Diallo, Kobbie Mainoo na Alejandro Garnacho kusalia Old Trafford, Arsenal wanalenga kumnunua Bryan Mbeumo msimu huu.
Winga wa Ivory Coast Amad Diallo, 22, amekubali masharti ya mkataba mpya na Manchester United. (ESPN)
Kiungo wa kati wa Uingereza Kobbie Mainoo, 19, na winga wa Argentina Alejandro Garnacho, 20, wote bado wana nafasi ya kuendelea kusalia Manchester United, licha ya wasiwasi wa kukiuka sheria za faida na uendelevu (PSR). (Sky Sports)
Manchester United inahitaji kufanya mauzo ili kufadhili uhamisho wa euro 60m (£50m) wa mlinzi wa Ureno na Paris St-Germain Nuno Mendes, 22. (Independent).
Mshambuliaji wa Brentford na Cameroon Bryan Mbeumo, 25, yuko kwenye orodha ya wachezaji wanaowania uhamisho wa majira ya joto. (Florian Plettenberg)
Vilabu vya Ujerumani Bayer Leverkusen, RB Leipzig, Mainz, Borussia Dortmund na Stuttgart zote zinamwinda kiungo wa kati wa Manchester City na Uingereza James McAtee, 22. (Telegraph – usajili unahitajika)
Manchester City bado wanamtaka Omar Marmoush, 25, mwenye thamani ya pauni milioni 50, lakini huenda wakapata shida kumzawadia mshambuliaji huyo wa Misri kutoka Eintracht Frankfurt mwezi Januari huku klabu hiyo ya Ujerumani ikipigania nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa. (Guardian)
Man City pia wanafikiria kumnunua beki wa Nottingham Forest na Nigeria Ola Aina, 28. (GiveMeSport)
Manchester United wana habari kuwa wawakilishi wa mshambuliaji wa Uingereza Marcus Rashford, 27, wanafanya mazungumzo na AC Milan. (Sky Sports)
Mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo anataka kuungana na mchezaji mwenzake wa zamani wa Manchester United Casemiro, 32, na ameomba klabu ya Al-Nassr kumnunua kiungo huyo wa Brazil. (Mirror)
Manchester City wamepiga haua katika mazungumzo ya kumsajili beki wa Uzbekistan Abdukodir Khusanov, 20. (Team Talk)
Winga wa Brazil Antony, 24, amekataa nafasi ya kujiunga na klabu ya Ugiriki ya Olympiakos lakini bado anataka kuondoka Manchester United. (Mirror)
West Ham wanavutiwa na kiungo wa Uingereza Kiernan Dewsbury-Hall, 26, na huenda wakashinikiza mkataba wa mkopo na Chelsea. (Independent)
Inter Milan wanaandaa ofa ya kumnunua mlinzi wa Ukraine na Arsenal Oleksandr Zinchenko, 28. (Sun)
Aston Villa inamfuatilia winga wa Borussia Dortmund Muingereza Jamie Jermaine Bynoe-Gittens, 20. (Caught Offside).