Nyota chipukizi Gavi na Lamine Yamal wameipeleka Barcelona fainali ya Spanish Super Cup kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Athletic Bilbao.. Dani Olmo alikosekana katika mchezo huo baada ya leseni yake ya kucheza kufutiliwa mbali,
Mchezaji wa Uhispania Olmo aliruhusiwa kucheza tena kwa muda kabla ya mchezo Jumatano, lakini uamuzi ulikuja kuchelewa sana kwake nafasi yake kuchukuliwa na Pau Victor.
Gavi aliiweka Barcelona mbele kwa shuti kali dakika ya 17 na winga kijana Yamal akafunga la bao la pili baada ya mapumziko.
Mabingwa wa Uhispania na Ulaya Real Madrid watamenyana na washindi wa pili wa kombe la Mallorca siku ya Alhamisi katika nusu fainali ya pili.
“Hatujali [tunakutana na nani kwenye fainali]. Itakuwa ngumu na tunataka kushinda, ambalo ni jambo muhimu, na kurejea nyumbani na kombe,” Yamal aliambia Movistar baada ya mchezo huo.
“Athletic ni timu ya kimwili ambayo inakufanya kukimbia sana. Tuliteseka zaidi hadi mwisho, lakini tuliweza kucheza vizuri, na tuna furaha sana, “Yamal aliongeza.
Fowadi mkongwe wa Kipolishi Robert Lewandowski alipoteza nafasi nzuri ya kuongeza la tatu, huku akipiga shuti kali akiwa katika nafasi nzuri.
Kocha wa Athletic Ernesto Valverde, ambaye alifutwa kazi kama mkufunzi wa Barcelona baada ya kushindwa katika uwanja huo mnamo 2020, alimleta Nico Williams kujaribu kubadilisha mchezo.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania, aliyehusishwa sana na Barcelona majira ya joto, hakuwa fiti vya kutosha kuanza, lakini alifanya vizuri kutoka kwa benchi.Winga huyo alimtengenezea Oscar de Marcos pasi nzuri ya mwisho lakini beki huyo wa Athletic alikuwa ameotea na bao lilikataliwa.
Barcelona walipata ushindi wao na kuwasubiri wapinzani wao katika fainali ya Jumapili, ambapo Olmo ataruhusiwa kushiriki.