Serikali imeombwa kuhakikisha inawakamata na kuwashughulikia Wafugaji wakorofi, ambao wamekuwa wakiwapiga Wakulima na kulisha mifugo katika mashamba yao yenye mazao katika maeneo mbalimbali hapa Nchini.

Ombi hilo, limetolewa na baadhi ya Wakulima katika Kijiji na Kata ya Magungu Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara, wakati wakiongea na Dar24 Media hivi karibuni na kudai kuwa hatua hiyo itasaidia kuondosha migogoro ya baina yao na Wafugaji.

Wamesema, Wafugaji wengi hasa wanaohamahama kutafuta malisho wanalalamikiwa na Wakulima kuwa ni chanzo cha uharibufu, ikiwemo matukio ya kuwapiga pindi wanapotetea haki zao baada ya kukuta Wenye mifugo wamelisha katika mashamba yao.

Jenifa Julius ambaye ni Mkazi wa kata hiyo, kwa upande wake alisema, “vitendo vya ubabe vinavyofanywa na baadhi ya wafugaji havikubaliki, hatuwezi kuwa na jamii ya namna hiyo na hivyo wale wote wanaofanya vitendo hivyo Serikali isiwavumilie Mkulima anaumia.”

Naye John Maziwi, ambaye ni Mfugaji amesema tangu enzi za kale hakukuwa na migogoro iliyokithiri kati yao na Wakulima kwani waliheshimiana na kuthamini cha mtu, lakini wahamiaji wamekuwa wakihamia na tabia zao mfukukoni wakitumia uhuru viobaya na kuleta taharuki.

Amesema, “na wala hatua tatizo sisi pia tunakula chakula kinacholimwa na Wakulima, lakini wenzetu hawa wasio na utambuzi kiukweli wanaturudisha nyuma na kukutoa thamani hata tusiokuwa na makosa hivyo wakishughulikiwa watatutofautisha kupata Wafugaji wenye weledi maana tupo.”

Malimwengu: Maswali mazito urafiki wa Chui na Ngombe
Watakiwa kuyaenzi, kudumisha mafanikio ya Serikali